- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Inaendelea....
UGONJWA
WA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCER DISEASE) KINGA,TIBA NA USHAURI
Ili kupunguza makali au kujiepusha
kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na
kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi
nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.
Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na
sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa
husababisha madhara mengi tumboni.
Hebu tuangalie aina ya vyakula
anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila
kusumbuliwa nao:
VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula
vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili
kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani
ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.
POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji
vingine vyenye ‘caffeine’, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya
tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka
au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza
asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa
anayeumwa.
ULAJI CHUMVI
Utafiti uliowahi kufanywa nchini
Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya
tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi,
hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike
haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.
MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri
wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats)
ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa
atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya
tumbo.
VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na
vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri
kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji,
ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi,
jibini na cream za maziwa huleta ahueni.
STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
Licha ya kusabisha Saratani,
uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya
tumbo, hivyo ni saba-bu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo
unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini
maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu,
hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu
kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.
Dawa ya vidonda vya tumbo (gastric and
duodenal ulcers)
i. Karela na mtindi
Majani ya karela 15 g
Mtindi glasi 1
Pondaponda majani ya karela, changanya
na mtindi.
Matumizi:
Glasi 1 kila siku kwa muda wa mwezi 1.
ii. Bilinganya.
Katakata bilinganya vipande vidogo
vidogo, chemsha na tia chumvi kidogo.
Matumizi:
Kula mara 2 kila siku kwa muda wa mwezi
1.
iii. Kabichi.
Kabichi ½ kilo
Maji ½ lita
Katakata kabichi vipande vidogovidogo,
tia maji na chemsha hadi maji yawe ¼ lita tu.
Matumizi:
Kunywa maji yote baada ya kupoa,
mara 2 kila siku kwa mwezi 1.
KUMBUKA: Kabichi lina kemikali
inayosaidia kuondoa vidonda vya tumbo
iv. Ndizi.
Ndizi 2 za kupika na maziwa glasi
1 mara 4 kama chakula pekee kwa muda wa siku 14.
v. Asali na Mdalasini
Asali na mdalasini inatibu maumivu
ya tumbo pia hutibu vidonda vya tumbo kwenye shina la vidonda.
vi. Karoti
MAANDALIZI;
Chukua karoti kilo1 ponda iwe
laini na kisha uchemshe kwa dakika 15 ndani ya maji lita 1 na nusu au mbili
chuja,kunywa juisi yake kwa kutibu vidonda tumbo au saratani ya tumbo,saratani
ya kizazi tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6. Dawa ingine ya
Vidond vya tumbo Vidonda tumbo:
Kula kipande cha papai kisichoiva
vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu
swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia
vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa
vidonda vimepona.
Kama kipato chako ni kidogo na
kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai
kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za
maji na kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya
mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani.
Comments
Post a Comment